KISIWA CHA ZUNIGA 1
"karibu Kisiwa cha Zuniga" ilikuwa ni Sauti kali iliyowapokea walipofunguliwa vitambaa vyeusi walivyokuwa wamefungwa usoni.hawakuelewa wamefikaje hapo kwani walikuwa wamefungwa vitambaa vyeusi machoni na mikono Yao ikiwa imefungwa minyororo wasiweze kutoroka kitu walichokumbuka pekee ni jinsi walivyochukuliwa toka majumbani mwao bila huruma.wakiwa bado wanazidi kushangaa tu yule mtu aliyewakaribisha alitoa amri wale watu waliokuwa wamekuja nao waliwachukua nakuanza kuende nao mahali ambako hawakupajua.Hii ilikuwa kama Sinema kwa vijana hao ambao walikuwa na majonzi na chuki kali juu ya serikali Yao ambao iliwanyima uhuru wao lakini hawakuwa na lakufanya kwani tiyari ilishawateke nakuwaleta mahali wasikokujua na kibaya zaidi wao wenyewe hawakujuana.
"sama-ha-ni una-kujua hu-ku" ilikuwa ni Sauti ya kijana wakike akimuuliza mwenzie aliyekuwa mbele Yake akijaribu kutafuta maswali ya majibu Yake kichwani.
"SIMA-M-A!!" ilikuwa ni amri kutoka kwa mwongoza msafara ambayo ilimshtua kila mmoja wao.
"HAIRUHUSIWI KUONGEA WALA KUNONG'ONA!! Kama una maswali utapata majibu Yake tukifika" baada yakumaliza kuongea ukimya ulichukua utawala miongoni mwa vijana walee huku hofu ikiwavamia mithili ya baridi LA mlimani kwani hakuna aliyejua nini hatima yake zaidi yawalio wachukua.nusu saa ilifika walikuwa wameshafika sehemu husika ambayo iliwashtua kwakweli kwani hawakuwahi kuona sehemu iliyovutia kama hiyo kwakweli ilivutia kwa muonekano kiasi kwamba wakajiuliza je raisi alijuwa kuhusu kisiwa hiki? Je ni kweli kisiwa hiki kiko Tanzania? Hakuwa na majibu. Si mandhari ya kisiwa hiko iliyoshtua Bali vijana wenzao waliowakuta ambao walikuwa kwenye mistari huku miili Yao ikidhihirisha afya njema kutokana nakunawiri. Wakiwa wanazidi kushangaa Mara wale vijana wenzao wakaanza kuimba nyimbo za sifa na ushujaa ambapo mstari moja ulionekana kutiliwa mkazo kiasi chakufanywa ndio kiitikio nao ulisema itumikieni nchi yenu mbaka kufa kwenu kwa wakati huo kiitikio hiko hakikuwasumbua Sana kwani bado hawakuielewa maana iliyofichwa ndani Yake.
"wenzenu wanawakaribisha piteni mbele kabisa"waliendelea kutembea lakini macho yalikuwa bado kwa vijana wale ambao waliambiwa ni wenzao kwanini ni wenzao? Na wawo waliletwa kama wao? Hakuna aliyepata majibu maswali haya yalikuwa magumu Sana kuyajibu ijapokuwa nyuso za vijana Hao ziliisaliti miili Yao yenye afya hawakuwa na furaha hadi pale walipolazimisha kufurahi mashavu Yao yalilizuia tabasamu lakweli kutoka hapo ndipo walipojua Kuwa walikuwa sehemu mbaya na wasingeweza toka.
Walifika mbele kabisa nakukuta vijana wenzao wengine wakiwa wameketi nyuso zao zikionyesha Hali yasintofahamu kama wao waliwatambua Kuwa na wao walikuwa wameletwa Leo wakiwa bado wanawashangaa wale waliona makundi mengine yakija nyuma walizidi kuchanganyikiwa huku wale wanaokuja nao wakiwa wameweka roho zao mikononi Kuna Muda walihisi labada wapo motoni wakisubiria huku Yao lakini lahasha haikuwa hivyo. Kauli ya ukimya iliwatesa Sana kwani waliitaji kupunguza mizigo ya maswali iliyoielemea akili Yao nakuichosha mioyo Yao lakini haikuwezekana iliwabidi wavumilie tu kwani ndo njia pekee na sahihi iliyobakia. Vijana walizidi kuletwa hatimaye wakaisha ndipo mlio WA ngoma uliposikika na kila mtu kutulia kama maji mtungini. Wakiwa wametulia waliwaona watu wakitoa salute kwa mtu ambaye hakuonekana vizuri baadaye watu wale walimpisha ndipo sura ya mheshimiwa ilipoonekana kwa vijana wageni hili lilikuwa jambo lakushtua lakini kwa wengine lilikuwa la kawaida Sana ama kweli heri Shari kamili kuliko nusu yake. Mheshimiwa alisogea nakusimama karibu na kipaaza sauti nakuanza kuongea.
"Vijana hamjambo!" waliitikia "hatujambo"aliendeleaa.."karibuni katika kisiwa cha Zuniga, kisiwa hiki ndo nyumbani kwenu na Familia yenu mpya. Kisiwa hiki kitawapa kila kitu na nyie mtakipa vitu viwili cha kwanza mwilini wenu wote na mwisho roho yenu kisiwa hiki hakitohitaji chochote zaidi ya hivyo na kama mlivyoambiwa kauli yetu ni kukaa kimya kuinua nchi yetu.kwa wale vijana wapya Leo mtapumzika kesho mtaanza kazi rasmi ikumbukwe hakuna kuuliza maswali yasiyohusiana na mwili wako ukikamwata sheria ya kisiwa cha zindiga itafuata mkondo wake na mwisho hakuna kurudi nyumbani tena wala msifikirie. Nishayajibu maswali yenu karibuni" mheshimiwa alimaliza nakuondoka zake lakini hakujibu swali lolote la msingi zaidi yakuwaongezea maswali na masikitiko mingine baada ya maneno ya mheshimiwa hakuna kijana yeyote aliyekuwa na nguvu hata yakuongea kila mtu alikuwa katika ulimwengu wake akiwaza nini kitakachofuata ilikuwa kama movie ambayo iliwaacha na maswali ambayo yangejibiwa na part 2 yake lakini part 2 ya maisha Yao katika kisiwa hiko sijui Nani ataweza angalua kuwapa vidokezo kwasababu mwenye mamlaka mwenyewe aliwapa vionjo.wakiwa wapo kwenye bumbuwazi bado walikuja wale viongozi walio wachukua nakuwapeleka sehemu zao zakulala ambazo zilikuwa nzuri na zakuvutia kwa wakati huo hawakuona uzuri wa sehemu hizo katakana na mawazo yaliyowaganda.
"kwa Leo mtapumzika mbaka kesho mtakapopata maelezo mengine" aliongea mmoja WA viongozi na Kisha wakaondoka.vijana walijilaza kila mtu kwenye kitanda chake akiwa na yake Moyoni na wengine kupitiwa na usingizi moja kwa moja mbaka walipokuja kuamushwa kwenda kula cha jioni. Miondoko Yao ilionyesha uchomvu na mkato WA tamaa hata walipofika sehemu ya kula walikuwa kama wafu wanaotembea licha yakuwakuta wenyeji wao.walichukua Chakula nakuketi mezani nakuanza kula hawakuchukua Muda kutokana nakupoteza hamu ya kula walirudi vyumbani mwao ambapo walichanganywa wavulana kwa wasichana na kisha kulala.
Usiku wakati kila mtu amelala fofofo kijana mmoja wakike alishtuka kutokana nakubanwa na haja ndogo,Giza LA nyumba hiyo ya kulala lilimpa uwoga mkubwa kiasi chakutamani amuamshe mtu amsindikize maliwatoni lakini upande mwingine wa fikra ulimwambia "hauna ndugu wala mtu yeyote unayemjua hapa unahisi watukasaidia ukizingatia wao wenyewe wageni na wanahofu kama wewe" ni upande huu WA fikra ndiyo ulimfanya achukue maamuzi magumu yakwenda mwenyewe. Alianza kutembea akigusa kitanda by kitanda mbaka alipofika mlango wakutokea nje ambapo aliushika nakuanza kuufungua Mara akasikia sauti za watu,mmoja akiongea kwa ukali na mwingine kwa huruma.
"UMEIVUNJA SHERIA YA KISIWA!!!" ilikuwa sauti ya mtu aliyepewa madaraka kijana yule wakike alibahatika kuiona sura ya mwanakisiwa huyo lakini yayule mnyonge hakubahatika bado alisahau hata safari ya maliwatoni.
"kifo ni hukumu yangu hata ukiniacha Hai ntauliwa tu nshatimiza kazi yangu" maneno ya yule mnyonge yaliufinya moyo WA kijana yule wa kike ambaye aliitaji maelezo Zaidi.akiwa bado kwenye tafakari yake aliuona mkono ukipita mbele yake nakuyaziba macho yake.kijana yule alishtuka nakujua kuwa ule ulikuwa mwisho wake.
"shshhh rudi kulala kabla ujaonekana"alimnong'oneza. Kijana yule aligeuka kumuangalia ni nani hakumuona mtu yeyote Hali hiyo ilimshtua zaidi nakumfanya aingiwe na hofu zaidi akiwa katika mchanganyikio huo anasikia mlio wa risasi unaomshtua nakumpelekea kuuachi mlango unaotoa kelele nakumshtua kiongozi yule,kijana yule anaona hana jinsi zaidi yakukimbia nakurudi kitandani kwake ambako hakukumbuki Ila Mungu si athumani mwanga wa mbalamwezi unamsaidia kumurika kitanda kilichowazi naye kujirusha kitandani hapo nakujifunika,kitendo cha yeye kujilaza kitanda Mara mlio wa switch unasikika Mara pap taa imewaka huku nyuma vishindo vya buti zilizostahimili vita zikisikika. Kijana yule amejikunyata ndani ya shuka huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa nguvu nakuumiza kichwa chake Muda wote aliombea miujiza hakuwa hata na mawazo ya mtu aliyemshika nakupotea.vishindo vya buti viliendelea kusikika vikisogea karibu na kitanda chake kijana yule alizidi kuombea miujiza nakumuahidi muumba kuwa hatorudia tena akiwa katika Sala yake hiyo alivisikia vishindo hivyo vikikwamia kwenye kitanda chake,kijasho chembamba kilianza kumtoka aliachana na Sala ya miujiza nakuanza kusali Sala ya kuombea kifo chema. Mara alihisi mkono ukiugusa mguu wake kwa nguvu.
"WEWEE!!" ilikuwa sauti ya ukali iliyofuata baada ya mkono kumgusa ilimshtua zaidi nakufanya haja ndogo imtoke papo hapo............ ITAENDELEA.

No comments