Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA
Godbless Lema, amefunguka kuhusu kitendo cha David Kafulila kuhama
CHADEMA na kusema ana amini atamshauri mke wake naye afuate nyayo zake.
Kwenye
ukurasa wake wa twiter Godbless Lema ameandika ujumbe akisema Kafulila
ni rafiki yake wa karibu, lakini kwa namna alivyoamua hana shaka
atamshauri mke wake ambaye ni mbunge kupitia chama cha CHADEMA, kufanya
kama yale aliyoyafanya.
"David Kafulila ni rafiki yangu, nafikiri kwa namna hii alivyoamua
ataweza bila shaka kumshauri Mbunge wa Chadema, Jesca Kishoa (mke wake)
kufikiri kama yeye, hii inaweza kusaidia maoni yake juu ya uamuzi
aliouchukua leo na kuthibitisha ukweli huu kama hupo", ameandika
Godbless Lema.
Hii leo David Kafulila ametangaza kukihama chama cha CHADEMA akidai
vyama vya upinzani havina nia ya kupambana dhidi ua ufisadi, lakini mke
wake Jesca Kishoa ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA bado
hajazungumza chochote.
KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu
No comments