AZAM YANASA MSHAMBULIAJI KUTOKA GHANA
Klabu ya soka ya Azam FC inayoshiriki
ligi kuu soka Tanzania bara imeanza usajili kwa nguvu baada ya jioni ya
leo kutangaza kumsajili mshambuliaji Bernard Arthur kutoka klabu ya
Liberty Professional ya Ghana.
Arthur
amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na timu hiyo inayoshika
nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu. Mchezaji huyo ametambulishwa
na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohammed, ambaye alisafiri hadi
nchini Ghana kukamilisha usajili huo.
Abdul ameeleza kuwa usajili wa Arthur mwenye miaka 20, ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la timu hiyo kwenye usajili huu wa dirisha dogo ambalo limefunguliwa tangu Novemba 15 na litafungwa Desemba 15.
Arthur amekuja kuziba pengo la straika mwingine, Yahaya Mohammed, aliyeondoka baada ya mkataba wake kusitishwa kwa makubaliano maalumu ya pande mbili wiki chache zilizopita.

KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu
No comments