-->

Header Ads

YANGA WALIAMSHA DUDE.. WATANGAZA USAJILI WA AJIBU RASMI.

Sasa rasmi klabu ya Yanga wametangaza usajili wa Ibrahim Ajibu baada ya tetesi za mda mrefu. Ajibu amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga.

Hata hivyo dau ambalo ameingiza Ajibu halijawekwa wazi ingawa taarifa kutoka kwa wadau wa karibu zinasema amesaini kwa milioni 50 na zawadi ya gari.

Inasemekana Yanga walimalizana na Ajibu mapema ingawa walishidwa kutangaza usajili wake sababu bado alikuwa na mkataba na Simba ambao umemalizika June 30.

Ajibu sasa atavaa jezi za Yanga rasmi huku akipewa Jezi namba 10 ambayo ilikuwa inavaliwa na Mateo Antoney


No comments

Powered by Blogger.