-->

Header Ads

SAMATTA NA ROONEY NGOMA DROO, GENK WAKIWAVAA EVERTON.

Katika muendelezo wa mechi za kirafiki timu zikijiandaa na msimu mpya timu mbali mbali zaendelea kukipiga katika nchi mbali mbali.

Jana Genk walikutana na Everton katika mechi ya kirafiki ambayo iliwakutanisha uso kwa uso mtanzania Mbwana Samata na Whyne Rooney.

Rooney akiongoza kikosi cha Everton alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Genk dakika 33 kabla ya mtanzania Samatta kufunga na kusawazisha goli hilo dakika ya 44.

Rooney ameendelea kuweka rekodi kwa kufunga mechi mbili za mwanzo akiitumikia Everton, goli la kwanza akifunga katika ardhi ya Tanzania dhidi ya Gor Mahia katika uwanja wa taifa huku Samata akitupia magoli matatu katika mechi nne za kujiandaa na msimu mpya.

No comments

Powered by Blogger.