KIGI MAKASI AFUNGA USAJILI SINGIDA UNITED.. KIKOSI KAMILI HIKI HAPA NI BALAA..
KIGI MAKASI AFUNGA PAZIA LA USAJILI SINGIDA UNITED FC.
Kigi Makasi, Winga huyu aliyehudumu kwa nyakati tofauti timu ya Taifa ya Tanzania, Simba S.C na baadae Ndanda Fc amekamilisha uhamisho wake kutoka Ndanda Fc kwenda Singida United Fc.
Kigj Makasi, Mchezaji anayeongoza kibongobongo kuwa na moyo wa kujituma vilivyo awapo uwanjani, ameamua kuivia beji ya ukepteni wa Ndanda Fc na kuelekea katikati mwa nchi ya Tanzania kuungana na timu ya Ushindi SU.
Kigi Makasi amekuwa ndio mchezaji anayefunga ukurusa wa usajili ndani ya Singida United kwa msimu wa 2017/2018.
Tulishamaliza kufunga Ukurasa wa wachezaji wanje(7players). 1.Elisha Muroiwa(Zimbabwe)
2.Twafadzwa Kutinyu (Zimbabwe)
3.Simbarashe Nhivi (Zimbabwe)
4.Wisdom Mtasa (Zimbabwe)
5.Shafik Batambuze(Uganda)
6.Dany Usengimana( Rwanda)
7.Michel Rusheshangoga(Rwanda)
Leo tumemaliza kusajili wachezaji wa ndani(9 players).
1.Atupele Green (Jk Ruvu)
2.Miraj Adam (Africa Lyion)
3.Kenny Ally (Mbeya City)
4.Roland Msonjo(Mshikamano Fc)
5.Pastory Athans (Simba)
6.Deus Kaseke(Yanga)
7.Ally Mustapha (Yanga)
8.Salum Chuku (Toto Africa)
9.Kigi Makasi (Ndanda Fc). Kwa taarifa yako, Kwa sasa Singida United ina jumla ya wachezaji 25.
Wachezaji 16 wamesajiliwa kutoka timu mbalimbali.
Wachezaji 9 ni wale waliosalia baada ya timu kupanda kucheza Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018.
Tunawashukuru vilabu mbalimbali ambao tulifikia makubaliano nao na wamewachukua baadhi ya wachezaji wetu walioipandisha timu, na baadhi ya wachezaji waliomba kuondoka kwa ridhaa yao.
Asanteni.
No comments