GUARDIOLA AENDELEA KUMWAGA FEDHA, ASAJILI MCHEZAJI HUYU KUTOKA REAL MADRID.
Baada ya kumaliza misimu uliopita bila kikombe chochote kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka, Guardiola amepania kufanya vizuri msimu huu.
Guardiola ameendelea kuimalisha kikosi chake kwa kufanya usajili wa bei mbaya baada ya jana kukamilisha dili la beki wa pembeni Danilo kutoka Real Madrid.
Danilo anakuja kuziba nafasi ya Kolarov ambaye aliomba kuondoka na kutimkia katika timu ya As Roma.
Manchester City kwa sasa ndo inakuwa timu yenye safu ya ulizi ya bei kali kuliko yoyote Uingeleza ikiongozwa na kipa ghali duniani Ederson, beki wa kati Stones, Mendy, Danilo na Walker aliyesajiliwa kutoka Tottenham.
No comments