-->

Header Ads

MSHIKAMANO CUP KILWA NI ZAIDI YA NDONDO CUP.. YATIKISA KUSINI.

Mshikamano cup kilwa.
Hii ni ligi ya mpira wa miguu, iliyoanza rasmi mwaka 2012. Ligi hii inafanyika kila mwaka mwezi wa saba katika mji wa kilwa kivinje, katika uwanja wa UKOTE mjini kilwa kivinje.
Washindi wa ligi hii tangu imeanzishwa.
2012- wauweni fc (kilwa kivinje).
2013- catalunya fc (Kilwa kivinje)
2014-macuzi academy (kilwa kivinje)
2015-haikufanyika kupisha uchaguzi mkuu.
2016-leicester city (kilwa Masoko).
2017-?.
Wadhamini: ligi hii inadhaminiwa na wadau wa soka mjini kilwa wakiongozwa na mratibu mkuu Ramadan Tella. Wakishirikiana na Chama cha mpira wa miguu kilwa KILFA.
Zawadi: mshindi wa kwanza hupata ng'ombe Wawili na jezi, mshindi wa pili na tatu huchukua mbuzi watatu na jezi mshindi wa tatu hupata mbuzi mmoja na jezi.
Licha ya hivyo kila timu inayofikia hatua ya robo fainali hupata pea moja ya jezi.
Zawadi za ziada: kila msimu wa ligi huwa na mfungaji bora, mchezaji bora na hata mchezaji mwenye kufunga mabao matatu (hat trick) hupata zawadi ya mpira.
Muitikio: watu zaid ya 1500 hujitokeza katika uwanja wa Ukote kuangalia ligi hiyo.
2017.
Msimu huu mpya umekua wa kipekee zaidi kwa vilabu vingi kujitokeza na muitikio umekua mkubwa zaidi.
Vilabu shiriki ni 16. Vipo kwenye makundi manne.
Kundi A. Macuzi academy
              Mtoni fc
              Miramba fc
              Kilwa youth
Kundi B. Catalunya fc
              Red star
              Al Qaeda songas
              Kivinje academy
Kundi C. Al Qaeda njia nne
              Kariakoo fc
              Arsenal fc
              Dogo dogo star
Kundi D. Leicester city
              Africa one
              Kago fc
              Funguni boys
*Leicester city ndio mabingwa watetezi wa msimu wa 2016. Waliifunga catalunya fc bao 1-0, timu hizo zilifungua ngao ya hisani iliyoisha kwa catalunya fc 2-1 Leicester city. 
Ziada: ligi hii inahusisha wachezaji wengi wa kubwa ambao wanashiriki kama vile Abdul seleman aliyekua na Serengeti boys u17. Underson laji aliyekua mchezaji wa Ashanti, anafi selemani wa namungo, mwalami maundu mlizi wa kushoto wa jang'ombe boys Zanzibar. Na wengine wa ligi daraja la kwanza.

SOURCE;
GHARIB MZINGA
HAFISA HABARI
klabu ya reicester city ambao ni mabingwa watetezi mshikamano cup kilwa.

kilwa youth.

macuz academy

kariakoo fc

Al queda

kivinje academy


No comments

Powered by Blogger.