MSHIKAMANO CUP; ARSENAL YAICHAPA DOGO DOGO STARS KILWA.
MSHIKAMANO cup kilwa.
Arsenal ya kijiji cha pande wilaya ya kilwa mkoani lindi imeinyuka dogo dogo star mabao 2 kwa 1, katika ligi ya mshikamano inayofanyika wilaya ya kilwa katika mji wa kilwa kivinje.
Magoli yalianza kipindi cha kwanza baada ya amanzi issa chollo kuipatia dogo dogo star bao la kuongoza dakika ya 35,
kipindi cha pili arsenal ilitoka nyuma na kusawazisha bao hilo dakika ya 55 kupitia mshambuliaji wake Omar murenda na dakika ya 70 mbaruku a mbaruku aliongeza la pili na kuifanya arsenal kushinda 2-1.
Arsenal kutoka pande wakiwa katika picha baada ya ushindi wao zidi ya Dogo dogo Star
matokeo hayo yamelifanya kundi C kusomeka kwa Njia nne kuongoza kwa point 3, wapili Arsenal, watatu Dogo dogo star na ya mwisho Kariakoo.
Dogo Dogo Stars kutoka Songo Songo wakitoka uwanjani baada ya mechi yao dhidi ya Arseno.
source;
Gharib Mzinga
Hafisa Habari


No comments