RASMI; OKWI AJIUNGA NA KIKOSI CHA SIMBA AFRIKA KUSINI.. NIYONZIMA KUTAMBULISHWA SIMBA DAY.
Kikosi cha Simba kimeelendelea kukamilika ambapo leo Emmanuel Okwi ameripoti katika kambi yao iloyofichwa huko Afrika Kusini.
Okwi alikuwa anasubiri Tunzo za Ligi kuu na azam nchini Uganda ili aweze kujiunga na Wenzake ambao walitangulia Afrika Kusini. Okwi alikuwa ametajwa kuwania kipengele cha mchezaji bora wa Azam ingawa hakufanikiwa kuchukua Tunzo hiyo.
Huku Okwi akiwa tayari amejiunga na kambi ya Simba bado mchezaji anayesubiliwa kwa hamu na mashabiki wa msimbazi, Haruna Niyonzima ambaye atatambulishwa siku ya Simba day.
Bado siku tisa kufikia Simba day ambapo kikosi rasmi cha Simba cha msimu ujao kitatangazwa. Dimba day itakuwa tarehe 8 mwezi wa nane.
No comments