-->

Header Ads

KASEKE AIKACHA YANGA NA KUTUA SINGIDA UNITED.

Kiungo wa pembeni ambaye aliyeitumikia Yanga msimu uliopita, Deus Kaseke ametua katika timu ya Singida kwa mkataba wa miaka miwili.

Kaseke ambaye bado alikuwa anahitajika na Yanga ila walikuwa wazito kutoa dau la milioni 50 ambalo mchezaji huyo alikuwa anahitaji ili kusaini mkataba mpya.

Singida tayari washakamilisha usajili wa wachezaji wawili wa Yanga ambao ni Kaseke na golikipa Ally Mustapha "Bartez" ambao wanaungana na kocha wao wa zamani Hans Van Pluijm.

No comments

Powered by Blogger.