KANYE WEST AMKINGIA KIFUA MKEWE KIM KARDASHIAN KUHUSU MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA
Mjadala huu ambao unamtuhumu Mke wa Kanye West ambaye ni Kim kardashian kwa utumiaji wa madawa ya kulevya ambao ulianzia kwenye mtandao wa Snap chat.
Kim Kardashian alipost video akiwa chumbani kwake lakini nyuma yake kulikua na meza iliyo onesha kuwa inavimistari viwili vya unga vinavoashiria ni Cocaine.
Baada ya mjadala huo kushika kasi Kim aliamua kwenda ukurasa wake wa Tweeter na kuonesha picha vizuri huku akidai kuwa sio madawa ya kulevya bali ni rangi ya meza ingawa watu walishindwa kumuelewa mwanamama huyo.
Lakini mume wa mwanamitindo huyo Kanye west ameibuka na kusema kuwa ni chuki za baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimpiga vita mke wake na kusema kuwa mke wake hatumii madawa ya kulevya.Vyanzo vya karibu vya wanandoa hao viluambia mtandao wa Hollywood life kuwa Kanye amekasirishwa sana na watu wanamtuhumu mke wake na kusema kuwa mtu anaemjua Kim Kardashian basi hawezi kuamini habari hizo ambazo sio za kweli
No comments