-->

Header Ads

DK. MAGUFULI-“Namaanisha nguvu za kufanya kazi, nguvu za kulima. SIO HIZO ”


 Rais John Magufuli amewalaani vikali wavuvi wanaomwaga dawa zenye kemikali hatari  katika vyanzo vya maji ili kupata samaki wengi na kusema kuwa tabia hiyo husababisha maradhi kama saratani na wanaume kuishiwa nguvu.

Rais ameyasema hayo leo (Jumanne Julai 4) wakati akizindua mradi wa maji Sengerema na kusema kuwa wavuvi hao wanaomwaga madawa kwenye vyanzo vya maji lazima wachukuliwe hatua.

Hata hivyo baada ya Rais kusema kuwa dawa hizo zinamaliza nguvu za wanaume na kuwafanya watu kucheka, alibadili ghafla usemi wake na kusema: “Namaanisha nguvu za kufanya kazi, nguvu za kulima.”

Alimtaka mkuu wa upelelezi na vyombo vya usalama kuhakikisha hakuna uvuvi haramu unaofanywa katika vyanzo vya maji.

No comments

Powered by Blogger.