-->

Header Ads

Chanel ten yarushiwa lawama kwa kumuonyesha Mkuu Wa mkoa Wa dar es salaam

Katibu wa  TEF Neville Meena 

Dar es Salaam. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesema kwamba uamuzi wa pamoja wa kutotangazwa kwa habari zozote zinazomhusu  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam bado haujatenguliwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam  leo   Katibu wa  TEF Neville Meena amesema kwamba TEF inakiri kutangazwa kwa habari za mkuu huyo wa mkoa zaidi ya mara moja  katika kituo cha Channel Ten, mara moja katika tukio la msiba lililorushwa na kituo cha Radio cha  EFM.

Pia amesema imekuwa  kawaida kwa vyombo vya kampuni ya Sahara (Star TV na Redio Free Afrika) kwa kuzingatia kwamba kufanya hivyo ni kukiuka makubaliano ya ushirikiano wa kitaaluma (Professional Solidarity) uongozi unalifanyia kazi suala hili.

Amesema kwamba Uongozi wa TEF unawasiliana na taasisi husika baada ya hapo itatolewa taarifa rasmi kuhusu matokeo ya mchakato huu.

Amesema kwa sasa wanapenda kuwakumbusha wahariri na waandishi wa habari kwamba makubaliano yaliyofikiwa kuhusu suala hili yako palepale hadi uamuzi ,mwingine utakapotanaghzwa.

“Tunaomba kuweka tuendelee kushirikiana katika kulinda uhuru wa taaluma yetu’’anasema

Alisema mtu ambaye amefungiwa kutokutangazwa habari zake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na siyo habari za Mkoa wa Dares salaam .

“Hii inamaanisha kwamba Habari zote za mkoa wa Dar es Salaam zisizomhusisha mkuu huyo wa mkoa ,zimekuwa zikiandikwa na kutangazwa”anasema Meena

Anafafanua kwamba habari zote na zile zinazohusu matatizo ,changamoto na maendeleo ya wananchi ,matukio ya kipolisi (Kanda Maalum na mikoa yote ya kipolisi) ,wakuu wa wilaya zote tano za mkoa huo ,mamlaka za mitaa kwa maana ya Halmshauri za manispaa zote , Halmshauri ya jiji la Dar es Salaam pamoja na Habari za Taasisi,Wizara ,Idara na vyombo vyote vya Serikali vilivyopo Dar es Salaam.

“Hivyo basi siyo kweli kwamba kutotangazwa kwa taarifa zinazomhusu Mkuu wa Mkoa ni kutotangazwa kwa habari za Mkoa huu ni upotoshaji unaofanywa kwa lengo la kuficha uovu ambao mhusika aliufanya kwa kuvamia chombo cha habari usiku akiwa na silaha’’anasema  Meena
Chanzo mwananchi


JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.