Kikosi cha kuivaa Rwanda mda mchache ujao hichi hapa.
Hiki ndicho kikosi cha Taifa Stars kitakachoivaa Rwanda mda mchache ujao.
Kocha wa Timu ya Taifa Stars, Salum Mayanga ametaja kikosi cha kwanza kinachoivaa Rwanda jioni hii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza huku mshambuliaji John Bocco akirejea kikosini.
Bocco aliongezwa kwenye kikosi hicho baada ya kuumia washambuliaji Mbarajka Yusuph na Shaban Idd.
Kikosi kamili kinachoanza ni Aishi Manula, Shomar Kapombe, Gadiel Michael, Salim Mbonde, Nurdin Chona,, Himid Mao, Erasto Nyoni, Simon Msuva, Mzamiru Yassin, John Bocco na Shiza Kichuya.
Mechi hiyo ya kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani inaanza saa 10 jioni hii.
Endelea kufuatilia mtandao wetu kupata taarifa zaidi.
No comments