-->

Header Ads

Viazi vya Limao na kitunguu Swaumu

RECCIPE SAFI KABISA YA KUPIKA VIAZI ULAYA VYENYE MCHANGANYIKO WA LIMAO NA KITUNGUU SWAUMU
MAHITAJI
4 vikubwa viazi ulaya, osha vizuri
3 kijiko kikubwa cha chakula olive oil
2 kijiko kikubwa cha chakula juice ya limao
2 kijiko kikubwa cha chakula majani ya korienda au giligilani
4 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu kilichosagwa
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI


Osha vizuri viazi kasha kata vipande vine kwa kiazi kidogo na vipande sita kwa kiazi kikubwa kata kwa urefu kama inavyoonekana kwenye picha, watu wengi huwa menya maganda ya viazi lakini mimi simenyi naacha maganda ili nisipoteze virutubisho au nutrient zilizojaa kwenye ngozi.


Washa jiko katika moto wa kati kisha weka vijiko viwili vya mafuta yapate moto, mafuta yakishapata moto weka viazi vyako kwenye kikaango


Hakikisha viazi vyako vinakua na rangi ya kahawia pande zote na pika kila upande kwa sakika 5 hadi 6 ndio safi.


Punguza tena moto uwe wa kati ili usiunguze, kisha funika mfuniko na acha viendelee kuiva ili viwe laini kabisa na safi kwa mlaji.


Wakati huo huo chukua bakuli safi kavu na uchanganye mafuta ya olive vijiko viwili , juice ya limao, majani ya corriender au gili gilani, kitunguu swaumu, chumvi na pili pili manga. Hakikisha unachanganya vizuri.


Baada ya viazi kuwa laini, chukua ule mchanganyiko wenye mafuta na mwagia kwenye viazi hakikisha unachanganya pole pole bila kuvivunja.


Toa mfuniko na kasha endelea kuvipika kwa dakika 3 hadi 4. wakati mzuri ni pale unapomwagia ule mchanganyiko wa mafuta na kitunguu swaumu ooohh ghafla italipuka harufu safi ya kuvutia pia viazi vitakua na ngozi ya kukauka na yakuvutia kama unavyoona kwenye picha.


 Unaweza ongezea majani ya giligilani au korienda kwani pia inahusika sana kwenye kuongeza ladha ya viazi hivi


Viazi hivi ni maarufu sana kwa nyama choma au samaki choma au kuku choma waandalie familia au wateja hotelini kwako na watafurahia sana sana, ni niafuu na rahisi sana kuandaa.




KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu

No comments

Powered by Blogger.