ABDI BANDA APATA DILI AFRIKA KUSINI, ATUA TIMU HII..
Beki kisiki wa klabu ya Simba na timu ya taifa Tanzania, Abda Banda ameongeza tetesi za kuondoka katika klabu yake aliyoitumikia msimu uliopita Simba na kutua katika timu BAROKA FC inayoshiriki ligu kuu ya Afrika Kusini.
Kurasa (account) rasmi ya Abdi Banda ya Instagram inasomeka kuwa Banda ni mchezi halali wa timu Baroka na kuongeza uvumi kuwa mchezaji huyo ameikacha rasmi Simba na kwenda kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini.
Ikumbukwe Banda aliomba kuondoka kati kati ya msimu baada ya kupoteza nafasi ya kucheza Simba. Baada ya mazungumzo alifanikiwa kutudi uwanjani ila hata hivyo nilikuwa na tetesi kuwa kuna timu moja ya Afrika Kusini ulikuwa inahitaji huduma take.
Baroka Fc ambayo inasemekana Banda amejiunga nayo ni miungoni mwa timu za mwisho katika ligi hiyo ambazo zilikuwa zikipambana kubaki ligi kuu.
kurasa (account) rasmi ya Abdi Banda inasomeka kama ifuatavyo.
No comments