Wajue wasanii wa Hip Hop wa 5 matajiri duniani.
Hivi karibuni jarida la forbes lilitoa orodha ya wasanii wa hip hop wanao ongoza kwa utajiri duniani.
Hii ndio orodha ya wasanii wa hip hop matajiri duniani
1)Diddy
Jina kamili ni Sean Comb ambaye anatajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 820 .
Sean Comb ambaye anajulikana kwa jina lake maarufu la puff diddy ni mfanya biashara na msanii mkubwa nchini marekani.Diddy ambaye ametajwa kuwa na uwezekano wa kuwa msanii wa kwanza kufikisha utajiri wa dola za kimarekani bilioni 1.
2)Jay Z
Jina kamili ni Shawn Carter ambaye ni mume wa msanii mkubwa nchini Marekani Beyonce Knowles,Jay z ambaye anatajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 810.
Jay Z ambaye ni mfanya biashara maarufu na mmiliki wa mtandao wa muziki wa Tidal yupo nyuma ya Diddy kwa tofauti ya dola milioni 10.
3)Dr.Dre
Jina lake kamili ni Andre Romelle Young anaetajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 740. Dr.Dre ambaye alijiongezea utajiri wake baada ya kuuza beats zake kwa kampuni ya apple.
4)Birdman
Bryan Williams ambaye anatajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 110.Birdman ambaye ni mmiliki wa lebo ya muziki ya cash money ambayo inamiliki wasanii Drake,Nick Minaj ,young thug na wengine .
5)Drake
Aubrey Drake Graham ambaye anajulikana kwa jina la Drake alitajwa na jarida la forbes kuwa ni rappa wa tano kwa utajiri duniani akiwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 90.
Drake ambaye amejizolea sifa nyingi sana kwa kutoa vibao vikali kama one dance na hotline bling vilivyomfanya atwae tunzo mbali mbali.
No comments