-->

Header Ads

TETESI; MSUVA AULA DILI LA BILIONI MISRI, NJIA NYEUPE KUONDOKA JANGWANI.

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Simon Msuva huenda akajivunia kitita cha pesa endapo kutapatikana muafaka baina yake na klabu yake ya sasa ili yeye apate kuelekea huko nchini Misiri kukipiga katika klabu ya Zamalek .

Imeelezwa kua Msuva huenda akajipatia sh.bilion 1.6 kama klabu  yake ya Yanga itamruhusu kuelekea huko,hata hivyo taarifa hizo zinaeleza kua nyota huyo endapo atasaina kandarasi na klabu hiyo atajipatia malipo ya Dora 15,000/- kwa mwezi ambayo ni sawa na shillingi  millioni 33.2.

Kuondoka kwake kunaweza kufungua njia kwa wachezaji wapya ambao inasemekana yanga wameshamalizana nao ambao ni Chanongo na wamemrudisha kipenzi cha wana Yanga, Mrisho Ngassa na kufanya njia ya Msuva kuondoka jangwani kuwa nyeupe.
Vile vile nafasi yake inaweza kuchukulia na Juma Mahadhi ambaye ameshindwa kumpa changamoto Msuvu au nafasi hiyo inaweza kuangua kwa kinda wa Yanga Yusuph Mhilu kama dili hilo litafanikiwa
Hata hivyo Msuva anahusishwa pia kuhitajika na mahasimu wa klabu ya Yanga "Simba" na klabu nyingie kutoka huko bondeni South Afrika.

No comments

Powered by Blogger.