MAKINDA WA YANGA WAUA SPORTS PESA, WAWAPA MTIHANI SIMBA.
Yanga imetinga nusu fainali ya Sports Pesa Super Cup kwa mikwaju ya penalti.
Yanga imeing'oa Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila bao.
Kikosi cha Yanga ambacho kilisheheni vijana kutoka Yanga B walifanya kazi ya ziada kuwazuia Tusker na kuwaweza kuwamudu kwa dakika tisini bila kufungana.
Kuondoka kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao wameungana na timu ya taifa kumewapa nafasi kina Mohammed Ally, Yusaph Muhilu na Said Mussa ambao waliweza kumudu nafasi zao kwa ufasaha.
Sasa Yanga itakutana na Wakenya wengine, safari hii ni AFC Leopards ambao wameing'oa Singida United kwa mikwaju ya penalti pia.
Simba nao wanatarajia kushuka dimbani kesho huku ikiwakosa pia wachezaji wake tegemezi kama Mkude, Kichuya, Tshabalala, Mzamiru na Ndemla ambao wanatumikia kikosi cha taifa
Huku Mavugo na Juuko Murshid hawapo nchini kwa sababu ya majukumu ya taifa. Hivyo Simba itawapasa kutumia kikosi cha pili na sura mpya ili kuziba mapengo ya wachezaji ambao watakosekana kesho.
No comments