-->

Header Ads

SABABU YA YANGA KUTOKUTANGAZA USAJILI WA IBRAHIM AJIBU HII HAPA..

Kuna watu bado hawaamini kama ajibu kasaini yanga, Taarifa ambayo imetufikia inasemekana Yanga hawawezi kuweka hadharani usajili wa Ajibu kwa maana bado ana mkataba na simba.

Endapo Yanga watatangaza usajili huo mapema, Simba wanaweza kuandaa malalamiko ya ajibu kwa maana bado Ana mkataba na simba ambao unafikia hitimisho June 30.

Inasemekana Yanga hawataki kuwapa simba hata nafasi ya malalamiko kama ilivyotokea kwa Hassan Kessy ambapo Yanga waliadhibiwa kuilipa klabu ya Simba milioni 50.

Inasemekana July mosi mambo yanakuwa hadharani na rasmi Yanga watamtangaza Ajibu kuwa mali yao. Viongozi wa Yanga wako makini, na Ajibu ni mali ya yanga ila mpaka mkataba wake utakapoisha mwezi huu ndipo wataweka mambo hadharani.

Inasemekana Ajibu amepokea kiasi cha milioni 60 na gari kama ushawishi wa kutua jangwani.

No comments

Powered by Blogger.