RONALDO AWEKA REKODI NYINGINE ULAYA MADRID WAKIWAFUNGA JUVENTUS


Magoli ya Real Madrid yalifungwa na Christian Ronaldo aliyekwamisha mpira wavuni mara mbili, dakika ya 20 na dakika 64. huku magoli mengine yakifungwa na Casamiro na Asensio dakika ya 90.
Ushindi huo umewafanya Real Madrid kuwa klabu ya kwanza kutetea ubingwa wa ulaya toka mwaka 1990 na huku ikiwa wanachukua kombe hilo kwa mara ya 12.
Vile vile Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora mara 5 mfululizo akiwa na magoli 12 akifuatiwa na Messi mwenye magoli 11. Rekodi nyingine aliyeweka Ronaldo ni kufunga goli kwa fainali 3 tofauti alizocheza katika michuano hiyo na vile vile ametimiza magoli 600 tangu aanze kucheza mpira wa kulipwa.
Wakati Ronaldo akiweka rekodi mbali mbali hali ni tofauti kwa Buffon ambaye mpaka sasa amepoteza fainali 3 huku matumaini ya kuchukua ubingwa huo yakipotea kutokana na umri kumtupa mkono.


No comments