-->

Header Ads

RASMI; SHOMARI KAPOMBE AMESAINI RASMI SIMBA, WATAMBA USAJILI BADO HAWA..

Baada ya klabu ya Simba kufanikisha kuwanasa John Boko na Aishi Manura kutoka Azam, leo wamejamilisha dili nyingi kwa kumsainisha kandarasi ya miaka miwili beki wake wa zamani, Shomari Kapombe

Beki huyo ambaye aliichezea simba kwa mafanikio amefanikisha dili hill ambalo linamrudisha kuwatumikia wana msimbazi kwa miaka miwili

Mpaka sasa Simba imefanikisha kunyaka saini za wachezaji watano ambao ni Aishi Manura, Kapombe na John Boko kutoka Azam. Wengine ni Yusuph Mpilipili kutoka Toto na Rasta Jamal Mwambeleko kutoka mbao.

Taarifa ambazo bado hazijithibitishwa kuwa Simba wanafanya juhudi kubwa kumshawishi Haruna Niyonzima kutua msimbazi ambapo inasemekana ameandaliwa kitita cha milioni 150.

No comments

Powered by Blogger.