-->

Header Ads

UKATA BADO TATIZO YANGA, AZAM WAWAFANYIA UMAFIA.. WASAJILI MCHEZAJI AMBAYE WALISHAMALIZANA NA YANGA..


Klabu ya Azam FC imemnasa mshambuliaji anayekuja kwa kasi hivi sasa nchini, Wazir Junior.

Junior aliyependekezwa na Kocha Mkuu Aristica Cioaba, anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao 2017-18, ambapo alikuwa straika kinara wa Toto African ya Mwanza msimu uliopita, akiwa mfungaji wao bora kwa mabao sita aliyofunga.

Awali mshambuliaji huyo alifanya mazungumzo na klabu ya Yanga ila walishindwa kufanikisha dili hilo kutokana na Yanga kukosa fungu LA kutosha katika usajili.

 Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa aliambiwa asubili fungu ambalo litapatikana kwenye michuano ya Sports Pesa kukamilisha dili hilo.


Klabu ya Azam waliingilia kati usijili huo na kufanya kwa haraka na hawakulaza hata usiku mmoja kukamilisha dili hilo na kufanikiwa kuwapiku wapinzani wao Yanga katika kuwania saini ya mshambulia huyo. Na rasmi ametambulishwa katika kikosi hicho tayari kwa kukitumikia katika msimu ujao.



No comments

Powered by Blogger.