HIVI NDIVYO RAYVANNY ALIVYOFANYA NGOMA YAKE MPYA NA JASON DERULO
Kushindwa kutumia fursa kwa kila nafasi unayoipata imekuwa ni dhambi kubwa kwa wasanii wa WCB. Hatimaye Rayvanny amekamilisha ndoto yake aliokuwa akiiota kwa muda mrefu.
Hitmaker huyo wa MBEREKO, ambaye siku chache zilizopita amenyakuwa tuzo ya BET, amefanikiwa kukamilisha kufanya kazi na Jason Derulo kutoka Marekani.
Kupitia mtandao wa Instagram, Ray ameweka picha akiwa syudio na msanii huyo na kuandika, “God bless you my brother @jasonderulo its amaizing opportunity,am so grateful for that……… Toka Saa 8 Usiku amekaa na mimi hadi Asubui… Studio kulikua na Watoto wakaaaaaliiiii 😂lakini kawacha waondoke sababu walichoka kukaa studio yeye kabaki na sisi tu. Naamini kilichofanyika Mtakipenda. Thanks boss @afrikidd @babutale.”
Baada ya wasanii hao kukamilisha kazi yao hiyo walijumuika pamoja katika kucheza mchezo wa mpira wa kikapu ambapo Ray alijikuta akiambulia za uso kutoka kwa Jason. Wawili hao kwa mara ya kwanza walikutana nchini Kenya kwenye Coke Studio Afrika wiki chache zilizopita.

No comments