-->

Header Ads

Hatimaye Mahakama Kuu ya Uganda imetoa amri kaburi la Ivan Ssemwanga, yule mtalaka wa Zari, lifukuliwe Haraka..

Inaelezwa kutoka Uganda:Hatimaye Mahakama Kuu ya Uganda imetoa amri kaburi la Ivan Ssemwanga, yule mtalaka wa Zari, ambaye ni mke wa sasa wa Diamond Platinumz lifukuliwe, ili mamilioni ya pesa alizozikwa nazo zitolewe.

Mahakama imesema imechukua uamuzi huo ili kulinda heshima ya fedha ya nchi hiyo.

Mahakama imechukua uamuzi huo baada ya Mganda mmoja aitwaye Mgugu Abey, kuwashtaki Mahakamani  kampuni iliyoratibu mazishi hayo ya A Plus Funeral Management na Benki Kuu ya Uganda,ambayo imeonekana ilizembea kwenye tukio hilo. 
Hivyo, mahakama imeamuru kampuni ivunje kaburi kwa gharama zao,ili mlalamikaji achukue pesa hizo kwa niaba ya mataifa yenye fedha hizo, kwani zilikuwepo Rand za Afrika Kusini,Dola za Marekani pamoja na Shilingi za Uganda.

Kisha kampuni ya A Plus imeamriwa ilifukie kaburi hilo kwa gharama zake  na kisha kumlipa ndugu Abey gharama zingine za usumbufu.

Inaelezwa kutoka Uganda: Hatimaye Mahakama Kuu ya Uganda imetoa amri kaburi la Ivan Ssemwanga, yule mtalaka wa Zari, ambaye ni mke wa sasa wa Diamond Platinumz lifukuliwe, ili mamilioni ya pesa alizozikwa nazo zitolewe.

Mahakama imesema imechukua uamuzi huo ili kulinda heshima ya fedha ya nchi hiyo.

Mahakama imechukua uamuzi huo baada ya Mganda mmoja aitwaye Mgugu Abey, kuwashtaki Mahakamani kampuni iliyoratibu mazishi hayo ya A Plus Funeral Management na Benki Kuu ya Uganda,ambayo imeonekana ilizembea kwenye tukio hilo.
Hivyo, mahakama imeamuru kampuni ivunje kaburi kwa gharama zao,ili mlalamikaji achukue pesa hizo kwa niaba ya mataifa yenye fedha hizo, kwani zilikuwepo Rand za Afrika Kusini,Dola za Marekani pamoja na Shilingi za Uganda.

Kisha kampuni ya A Plus imeamriwa ilifukie kaburi hilo kwa gharama zake na kisha kumlipa ndugu Abey gharama zingine za usumbufu.

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa

No comments

Powered by Blogger.