-->

Header Ads

VYETI FEKI VILIVYOMNG'OA MUHUDUMU WA MOCHWARI..INAUMA SANA..

Sakata la vyeti fedha limemuondoa kazini mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti wa hospitali ya Mkoa wa Shinyanga baada ya kukutwa na cheti cha kughushi.

Katibu tawala wa Shinyanga, Albert Msovela amemtaja mtumishi huyo kuwa ni Christopher Lwambo na kusema kuwa ndiye pekee katika hospitali hiyo aliyebainika kuwa na cheti feki.
Msovela amesema hakuna mtumishi mwingine wa umma katika taasisi hiyo aliyenaswa na cheti bandia na kwamba, huduma zinaendelea vizuri.
Wakati mtumishi huyo akiondolewa, Mwenyekiti wa CCM wilayani Chamwino, Charles Ulanga ambaye ni mratibu wa elimu wa Kata ya Buigiri ameandika barua ya kukata rufaa lakini ametakiwa kuipeleka kwa mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri.
“Nilishaandika barua, lakini tulielekezwa kuzipeleka kwa waajiri wetu ambao wao ndiyo watazifikisha kwa wahusika. Mimi nimeshafanya hivyo,” amesema Ulanga.
Jina lake lilikuwa miongoni mwa majina yaliyojitokeza katika orodha ya watumishi wanaodaiwa kughushi vyeti.
Hata hivyo, alijitokeza hadharani na kupinga suala hilo akisema alisoma elimu ya msingi na baadaye ualimu bila ya kupitia elimu ya sekondari na kuwa ndivyo vyeti alivyowasilisha.
Wakati Ulanga akikata rufaa, Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (Talgwu) mkoani Morogoro kimepokea wafanyakazi zaidi ya kumi wakilalamikia kutotendewa haki.
Katibu wa Talgwu mkoani humo, Lawrence Mdega amesema wafanyakazi hao walifika ofisini kwake wakilalamika kuwa waliajiriwa kwa elimu ya darasa la saba, lakini wanashangaa wameandikwa kuwa walimaliza kidato cha nne.
Mkuu wa kitengo cha utawala na fedha wa Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua), Yonica Ndaga amesema watumishi watatu wa chuo hicho wameonyesha nia ya kukata rufaa wakidai kuonewa na uhakiki uliofanyika ambao haukuwatendea haki.

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.