-->

Header Ads

HIVI NDIVYO CHELSEA WATAKAVYOPOTEZA UBINGWA

Baba la ligi zote ulimwenguni kwa ushindani na kuwa na mashabiki wengi, ligi kuu ya Uingereza inaelekea ukingoni. 

Tottenham Hotspur wameteleza apo jana baada ya kufungwa na West Ham United 1-0 na kupunguza matumaini ya vijana hao wa London kunyakua taji la ubingwa wa ligi kuu. Manuel Lazini alifumania nyavu dakika ya 65 na kuwapa West Ham ushindi huo ambao umewapa ahueni timu ya Chelsea ambayo iko kileleni. \

Tottenham wanabaki nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi nne na kinara wa ligi huku wakiwa wamecheza mchezo mmoja zaidi ya wanaLondon wenzao hao. Mechi tatu za Tottenham ni sawa na pointi tisa (9) ambazo ukijumlisha na pointi 77 ambazo wanazo kwa sasa, watakua na jumla ya pointi 86. Hii ina maana kuwa Tottenham inaombea Chelsea ipate sio zaidi ya pointi 5 kwenye michezo minne iliyobaki ili watangazwe kuwa mabingwa. 

 Kwa hesabu hizi, Chelsea ikipoteza michezo miwili kati ya minne na ikatoka sare michezo mingine miwili basi The Blues watakuwa wamekabidhi ubingwa kwa Tottenham. Kwa aina ya ubora ambayo timu ya Chelsea imekuwa nayo kwenye msimu huu wa ligi, ni vigumu timu hiyo kutopata walau pointi sita ambazo zitawahakikishia ubingwa bila kujali matokeo ya timu zingine. Usiku wa jumatatu tarehe nane, 

Chelsea itawakaribisha Middlesbrough kwenye uwanja wa Stamford Bridge katika mechi ambayo itatoa mwanga mpana iwapo vijana wa Antonio Conte watatwaa taji la ligi. 

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA 

 Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.