-->

Header Ads

UBINGWA BADO KIZAZAA, SIMBA WAGOMEA ZAWADI WATUA FIFA.

Licha ya Yanga kukabidhiwa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, Jumamosi hii, upande wa pili ni kuwa Simba wameamua litakalokuwa na liwe.

 Taarifa ni kuwa uongozi Simba umesema hautambui ubingwa wa Yanga kwa kuwa waliomba kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wasimtangaze bingwa hadi hatma ya kesi yao ya kupinga kupokwa pointi 3 za mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar itakapoamuliwa.

Simba ilikata rufaa kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupinga pointi hizo ambapo kama ikizipata basi yenyewe ndiyo itatwaa ubingwa licha ya kuwa tayari upo mikononi mwa Yanga.

Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' amethibitisha kuwa barua yao imeshafika FIFA baada ya wao kukamilisha mchakato wa kuituma hivi karibuni.

Simba imesema kuwa kama rufaa yao itakataliwa au watashindwa basi wataipongeza Yanga kiroho safi ila siyo sasa.

No comments

Powered by Blogger.