-->

Header Ads

TETESI: - BALE KUHAMIA MANCHESTER UNITED

Gareth Bale, nahodha wa timu ya taifa ya Wales anaweza kurejea kwenye ligi kuu nchini Uingereza msimu ujao.

Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa mchezaji huyo anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ameshawasiliana na kocha wa Manchester, Jose Mourinho na wamekubaliana baadhi ya mambo yanayohusu uhamisho wa Bale kutoka Santiago Bernabeu hadi Old Trafford. Kabla ya kuhamia Madrid kwa ada ya rekodi ya dunia mwaka 2013, Bale alikua mchezaji tegemeo wa timu ya Tottenham Hotspurs.

Manchester United pia wanawania saini ya mchezaji wa Burnley, Michael Keane. Hata hivyo, United wanatarajia upinzani mkali kutoka kwa majogoo Liverpool ambao nao wanahitaji huduma za mchezaji huyo mwenye miaka 24 anasemekana kufikia makubaliano ya awali na meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers lakini anasubiri mpaka timu hiyo ijihakikishie nafasi ya kucheza klabu bingwa msimu ujao.

Tetesi zingine zinamhusu beki wa Southamptom Virgin Van Dijk anayehusishwa na klabu nyingi zikiwemo Chelsea na Liverpool. Meneja wa Southampton, Claude Puel amesema mlinzi huyo haendi kokote licha ya tetesi nyingi za kuhamia timu kubwa zaidi.

Puel amesema klabu ya Southampton haina lengo la kumuuza Mholanzi huyo mwenue miaka 25. Everton wao wako kwenye mbio za kunasa saini ya mchezaji Jordan Pickford kabla ya timu nyingine kuanza kumhitaji na kuongeza thamani yake kwenye soko.

Everton wametenga pauni milioni 10 lakini klabu ya Sunderland inataka pauni milioni 20 ili kumuachia Pickford. 

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA

 Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.