Sababu ya Wizara ya Fedha kuliomba Bunge Sh 11.7 trilioni
Wizara ya Fedha na Mipango imeliomba Bunge iliidhinishie
Sh11.757trilioni ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha
2017/2018, kwa mafungu yote tisa yaliyo chini ya Wizara hiyo.
Maombi
hayo yametolewa leo na Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mpango, wakati
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaya hiyo, Bungeni
Mjini Dodoma.
Dk Mpango amesema kuwa kati ya fedha
hizo, Sh10.328trilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na
Sh1.429trilioni ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Amefafanua
kuwa matumizi ya kawaida yanajumuisha Sh87.996bilioni kwa ajili ya
mishahara, Sh778.6bilini kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC) na
Sh9.4trilioni ni kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa na Huduma nyingine.
Pia katika fedha za matumizi ya maendeleo, Sh1.382trilioni ni fedha za ndani na Sh46.1bilioni ni fedha za nje.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments