-->

Header Ads

MAJEMBE NANE KUSEPA YANGA, NIYONZIMA NA NGOMA WATAJWA KUTUA MSIMBAZI.

Wachezaji 10 wa klabu ya Yanga wakiwamo nane wa kikosi cha kwanza mikataba yao ya kuichezea klabu hio imemalizika hivyo wanasubiri ripoti ya kocha, Lwandamina kama bado anawahitaji katika kikosi chake

Wachezaji wa tano mikataba yao imemalizika jana ambao ni Vincent Bossou, Kamusoko, Oscar Joshua, Matheo Antony, pamoja na Mwiji Haji.

Wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza wakiwemo Ngoma, Tambwe, Dida, Niyonzima na Kaseke mikataba yao inamalizika mwishoni mwa mwezi ujao.

Inasemekana klabu ya Simba imewaka katika rada zao kuwania saini wachezaji wa Yanga ambao wamemaliza mikataba yao. Wachezaji waliotajwa ni Niyonzima na Ngoma ingawa uongozi wa Simba hawajaweka bayana nia yao ya kuwasajili kuogopa hujuma.

No comments

Powered by Blogger.