Polisi wazingira mgodi wa Bulyanhulu
Jeshi la Polisi limeuzingira mgodi wa Bulyanhulu baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellaack kuzuiwa kuingia katika mgodi huo alikokwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA).
Jeshi hilo limefanya hivyo baada ya Tellack kuagiza kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anyetoka wala kuingia.
Mkuu huyo wa mkoa alitembelea mgodi mwingine wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia kama ulivyo ule wa Bulyanhulu.
Katika mgodi wa Buzwagi, Tellack na msafara wake waliruhusiwa kuingia na kishuhudia shughuli za uchimbaji ukiwa umeshitishwa kwa kukosekana maofisa wa TMAA walioondoka mara baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja bodi na kutengua uteuzi wa watendaji wakuu wa wakala hiyo.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments