-->

Header Ads

MAJINA YA WALIOKUFA KWA AJALI YA MUHEZA HAYA HAPA..INASIKITISHA




Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha Tumbo

Miili ya abiria waliokufa katika ajali iliyotokea juzi  saa 2.45 usiku baada ya basi aina ya Coaster walilokuwa wamepanda kuligonga lori wameanza kutambuliwa kufuatia  ndugu zao kujitokeza katika hospitali ya teule wilayani hapa.

Basi aina ya Coaster lililokuwa likitokea Jijini Tanga kuelekea mjini Muheza liligonga lori aina ya Scania lenye tela lililokuwa limeegeshwa pembeni katika kijiji cha Lusanga, barabara kuu ya Tanga-Segera na kusababisha abiria wanne kufa na wengine 13 kujeruhiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha Tumbo aliiambia Mwananchi kwamba hadi jana mchana miili  ya abiria wawili kati ya wanne waliokuwa wamehifadhiwa katika hospitali hiyo ilikuwa imetambuliwa na ndugu zao.

Aliwataja  waliokufa na kutambuliwa na ndugu zao kuwa ni  Ummy Amiri (28) aliyekuwa mkazi wa Kijiji cha Tingeni  pamoja na Nassib Salim (18) aliyekuwa mkazi wa Kitongoji cha Ngorongoro  Wilayani  hapa.

Majeruhi wa ajali hiyo ambao  wote wanapata matibabu katika hospitali ya teule kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya ni  Abdallah Majid (37), Mlondwa Guge (44), Twahiru Sebarua(35)  na Shaaban Abbas (21).

Majeruhi wengine ni Festo Asilia (35), Abdillah Fungo (32), Ali Mohamed (30), Isihaka Hassan (27), Ibrahim Bilal mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka mitatu hadi mitano, Magreth Tito (35) na Ummy Omary (23).



CHANZO: Mwananchi
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.