-->

Header Ads

KUFUTWA KWA MANENO HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI YAACHA TAHARUKI BUNGENI


Hotuba ya kambi ya upinzani imehaririwa kwa maelekezo ya Spika, Job Ndugai na kuondoa maneno kwenye kurasa namba 4, 7 na 19.

Kabla Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema Lema hajaanza kusoma hotuba hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga amesoma maelekezo ya Spika kuwa maneno hayo yafutwe na yasisomwe kwa sababu yalikwishazuiliwa katika hotuba zilizotangulia.

Alipofika kwenye maneno hayo akaanza kusema "Tatizo la rushwa..., amezimiwa kipaza sauti na kuelezwa na Giga kuwa suala hilo limeondolewa.”

Wabunge kadhaa walitaka kuomba mwongozo wa utaratibu lakini mwenyekiti akawakatalia.


CREDIT : Mwananchi

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.