-->

Header Ads

HIZI HAPA TETESI ZA USAJILI BARANI UTAYA, GRIEZMAN KUTUA OLD TRAFFORD

1.CHELSEA itamtoa kwa mkopo beki wake Kurt Zouma msimu ujao ili waweze kumsajili beki wa kati wa Southampton, Virgil Van Dijk. (#Telegraph)·

2.MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amekubali kutua Katika Viunga vya Old Trafford kwa Mshahara wa pauni £280, 000 kwa wiki baada ya klabu yake kupoteza muelekeo katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.(#Sun)·

3.KLABU ya Hoffenheim ya Ujerumani imeanza mazungumzo na Manchester City juu ya nia ya kutaka kumsajili Mshambuliaji wa Nigeria, Kelechi Iheanacho. (#OwnGoal_Nigeria)·

4.MAJOGOO wa Anfield Liverpool inataka kumsajili Kiungo wa Chelsea, Francesc Fabregas ambaye anatakiwa na Ac Milan. (#Daily_Star)·

5.BARCELONA bado hawajakata tamaa katika harakati zao za kutaka kumsajili Kiungo Mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho. Miamba hiyo ya Camp Now imepeleka ofa ya pauni £51m ili kumtwaa kiungo huyo. (#Sports)·

6.PSG inataka kumchukua kocha wa Zamani wa Manchester City, Roberto Mancini ili kuchukua nafasi ya kocha wao Unai Emery aliyefeli klabuni hapo. (#Son_Balon)·

7.MANCHESTER UNITED inataka kumsajili Kipa wa Ac Milan, Gianluigi Donnarumma ili kuchukua nafasi ya kipa wao David De Gea ambaye yupo mbioni kujiunga na Real Madrid. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 18 amekuwa katika kiwango cha juu kiasi cha kusakwa na klabu vigogo barani ulaya. (#Calciomercato)·

8.BAYERN MUNICH imeanza mazungumzo na Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez ili kujiunga na miamba hiyo ya Allianz Arena.Staa huyo amebakiza miezi 12 katika mkataba wake. (#Daily_Mirror)·

9.MANCHESTER CITY bado wanakomaa na Winga wa Bayern Munich Kingsley Coman. Staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa amesaini mkataba wa kudumu na wababe hao lakini City kupitia kwa kocha Guardiola wanataka kutoa pauni £50m wakiamini kuwa watampata. (#Times)·

10.MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Nolito anataka kurejea La Liga kwenye klabu yake ya Celta Vigo baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza mbele ya makinda, Raheem Sterling na Leroy Sane. (#Mirror)·

11.NYOTA wa Southampton Ryan Bertrand amewaambia viongozi wa klabu hiyo kuwa anataka kuondoka klabuni hapo huku Chelsea na Liverpool wakipigana vikumbo kuiwania saini ya nyota huyo ambaye aliwahi kukipiga Stamford Bridge. (#Daily_News)·

12.MSHAMBULIAJI wa Chelsea Diego Costa anakaribia kujiunga na Klabu ya Tianjin Quanjian ya China. (#Cadena_Ser)·

13.KIUNGO wa Liverpool Giorgion Wijnaldum yupo kwenye orodha ya nyota wanaotakiwa na Real Madrid. (#Tuttomercatowebb)·

14.ARSENAL itamsajili kiungo wa Malaga, Pablo Fornals kama mbadala Wa Santi Carzola. Gunners watatoa pauni £12m (€10. 1m)·

No comments

Powered by Blogger.