-->

Header Ads

KUFURU ILIYOFANYWA KWENYE BIRTHDAY YA CHRIS BROWN

Ameimba nyimbo kali kama Super human, With You, I can Transform Ya, Beautiful People, Kiss Kiss, Say Goodbye, Crawl, Yeah 3X, Loyal, Look at me Now, Right Next to You na nyingine kibao.

Amefanya collabo na wasanii wakubwa kama Lil Wayne, Busta Rhymes, Rihanna, Kery Hilson, The Game, T.I, Nicky Minaj. Ana albamu saba hadi sasa, albamu yake ya nane inatarajiwa kutoka mwezi ujao.

 Alipozaliwa wazazi wake walimpa jina Christopher lakini dunia nzima inamfahamu kama Chris Brown, mtunzi wa nyimbo, mwanamuziki, densa, muigizaji, mtayarishaji wa muziki, muongozaji video na mchoraji.
Ameshinda zaidi ya tuzo 80 ndani ya miaka 11, sura yake ni mmoja kati ya sura zinazotumbulika sana na kutumika ulimwenguni. Chris alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1989 huko Tappahannock - Virginia Marekani, akiwa na miaka 15 tu alipata mkataba wa kurekodi kutoka Jive Records na mwaka mmoja baadae alitoa albamu yake ya kwanza "CHRIS BROWN" ambayo iliuza nakala zaidi ya milioni tatu.
Dunia ilimchukia Chris Brown mwaka 2009 baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenzi wake ambaye pia ni msanii maarufu, Rihanna. Stesheni nyingi za radio na TV ziligoma kupiga nyimbo zake lakini kwa kuwa ni Chris Brown, alirudi kwenye chati baada ya kupigania nafasi yake katika muziki. Chris anasheherekea siku yake ya kuzaliwa leo, angalia video yake "PRIVACY" hapa chini.

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA
 Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.