-->

Header Ads

YANGA YATAJA SABABU KUCHEZESHA KIKOSI CHA PILI DODOMA, WATUPIA LAWAMA TFF.

TAARIFA KWA WANAHABARI NA WANA YANGA.
KUMEKUWA NA MKANGANYIKO WA HABARI NA UPOTOSHWAJI WA TAARIFA, AMBAZO SI SAHIHI KUHUSIANA NA YANGA KUCHEZESHA 
KIKOSI CHA PILI HAPO JANA DHIDI YA KOMBAINI YA MAJESHI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA.
NAOMBA KULIWEKA JAMBO HILI WAZI NA KUONDOA SINTOFAHAMU ZISIZO NA MSINGI NA PENGINE KUFUNGA MJADALA HUU RASMI.
1.WEEK END YA TAREHE 22 NA 23 ,NA YA 28 HADI 30 TFF WALITUPA RATIBA AMBAYO INAONYESHA HAKUNA MCHEZO WOWOTE LOCAL LEAGUE,
AU FA CUP.NA RATIBA YETU ILIONYESHA TUTACHEZA TAREHE 22 FA CUP DHIDI YA PRISONS TU KWA KUWA NI KIPORO,NA UKIANGALIA NI WIKI YA PILI SASA LIGI HAICHEZWI KUTOKANA NA RATIBA YA CHAN YAANI MASHINDANO YA KIMATAIFA YA CAF KWA TIMU ZA TAIFA KWA WACHEZAJI WA NDANI.
2.BAADA YA KUPATA RATIBA YA MAPUMZIKO YA WIKI MBILI BILA MICHEZO YA USHINDANI ,KAMA VIONGOZI TUKAONA SI BUSARA WACHEZAJI WAKAE BILA MICHEZO YA KUJIPIMA NGUVU ILI KUENDELEA KUJIJENGA KUWA KATIKA USHINDANI MUDA WOTE.
TUKAONA WIKI MBILI NI NYINGI MNO BORA TUPATE MICHEZO YA KUJIPIMA NGUVU YAANI FRIENDS MATCHES KATIKA MAJUMA HAYA MAWILI.
TULIPOKEA BARUA KUTOKA ARUSHA TUCHEZE MECHI MBILI TAREHE 29  NA 30 DHIDI YA MADINI NA AFC,TUKAKUBALIANA NAO PIA TUTAENDA HUKO.
TUKAPOKEA BARUA YA DODOMA TUCHEZE TAREHE 26 TUKAKUBALI PIA.
SASA TATIZO LIMEKUJA KWA TFF KUFANYA DROO TAREHE 23 ,NA KUTUTAKA TUCHEZE TAREHE 30 NUSU FAINALI YA FA CUP RATIBA AMBAYO HAIKUWEPO KABLA YA HAPO ,SISI TULIKUBALI KUCHEZA MICHEZO HIYO TUKIJUA HAKUNA MASHINDANO YOYOTE NDANI YA TAREHE HIZO.
3.NAKIRI KABISA KUWA TATIZO LIMESABABISHWA NA RATIBA ZISIZOELEWEKA ZA TFF TUSINGEFIKA HAPO,
KAMA RATIBA YA TFF INGEKUWA SI KUKURUPUKA TUSINGEFIKA HAPO LEO.
TUMECHEZA MECHI YA KIPORO NA PRISONS TUKASHINDA HUKU TUKIWA NA MAJERUHI WANANE KEY PLAYERS.
BOSOU
NGOMA
NIYONZIMA
JUMA ABDUL
BUSUNGU
BHATEZ
KASEKE
MATEO
SIKU YA PILI RATIBA INATOKA TUCHEZE NUSU FAINALI,NARUDIA TENA NUSU FAINALI TUCHEZE NDANI YA SIKU SABA.
KWA VYOVYOTE VILE HATA INGEKUWA VIPI ,KWA KIKOSI TEGEMEZI CHA WACHEZAJI 18 TU,KUKICHU KUA NA KWENDA KUKIPIGANISHA KATIKA MICHEZO MIWILI MFULULIZO AMBAO MMOJA HAUNA TIJA KABISA TENA MICHEZO HIYO IPISHANE KWA SIKU TATU TU, HII HAIJAWAHI FANYWA NA TIMU YOYOTE DUNIANI.
4.KWA KULIONA HILO NA KWA MAPENZI YA DHATI KABISA KUTOKA MIOYONI MWETU VIONGOZI DHIDI YA WAPENDA MPIRA WOTE WA MKOA WA DODOMA NA MAENEO YA JIRANI,VIONGOZI KWA PAMOJA SOTE TULITAFAKARI TUKASEMA KHERI YA NUSU SHARI KULIKO SHARI YENYEWE ,KWA PAMOJA TUKAHAMUA KUPELEKA TIMU YA KIKOSI CHA PILI WAKICHANGANYIKA NA WALE WA KIKOSI CHA KWANZA AMBAO HAWAJATUMIKA MUDA MREFU WAUNGANE NA VIJANA HAO KWENDA KUWAPA BURUDANI WANANCHI WA KANDA YA KATI DODOMA.
5.NASHUKURU TIMU IKIONGOZWA NA MIMI MJUMBE MKEMI,MJUMBE HASHIMU NA MJUMBE SIZA IMEFIKA SALAMA NA BADO IPO SALAMA SALMIN NA JANA IMEONYESHA KIWANGO CHA JUU KABISA NA WALE WALIOKUWA HAWAAMINI WALIACHA VITI VYAO NA KUSHANGILIA SOKA SAFI NA MARIDADI LA VIJANA WA YANGA ,MPAKA NIKAWATANIA VIJANA NI HALI HII WANGEKUJA BABA ZAO NDIYO MSINGEKAA VITINI MUDA WOTE.
KWA MACHACHE NI HAYO ILA NA PELEKA PONGEZI KWA BENCHI LA UFUNDI LA YANGA B CHINI YA KOCHA SHADRACK MSAJIGWA KWA KIWANGO BORA KABISA CHA TIMU YAKE AMEWAPIKA VIZURI HAKIKA HIKI NI KIKOSI HADHINA MARIDHAWA YA YANGA HAPO BAADAE.
NITAKUWA MCHOYO WA FADHILA KWA PATO NGONYANI ALIKUWA CAPTAIN JANA KIWANGO KIZURI HAKIKA ANARUDI SASA.
YOTE KATIKA MWISHO PONGEZI KUBWA, NZURI SIFA KEDEKEDEE KWA YUSUF MHILU MFUNGAJI BAO LA KUSAWAZISHA DHIDI YA MAJESHI,SIYO SIFA HIZI KWA AJILI YA GOLI TU LA HASHA HAKUNA ALIYEKAA BILA KUTOA YOWE LA FURAHA KILA ALIPOSHIKA MPIRA, HUYU NI MESSI WA TANZANIA KWA VIZAZI VIPYA VYA MPIRA TANZANIA.
MWISHO KABISA NALIOMBA SHIRIKISHO LA MPIRA TANZANIA TFF LIWE LINATOA KALENDA AU RATIBA AMBAZO BAADAE HAZITALETA MITAFARUKU KAMA HII HAPO BAADAE .
YANGA OYEEE
DAIMA MBELE 
NYUMA MWIKO

SALUM MKEMI
MJUMBE KAMATI YA UTENDAJI YANGA.
MSIMAMIZI MKUU WA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO YANGA.

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA

No comments

Powered by Blogger.