-->

Header Ads

IFAHAMU NCHI WANANCHI WAKE WANAOKULA MBWA NA PAKA




Mdau na msomaji wa AKISITV bila shaka wengi tunaishi na mbwa na paka katika familia zetu kama walinzi na moja ya wanafamilia.
Lakini hali iko tofauti kwa nchi nyingine duniani, hapa nazungumzia taifa la Taiwan ambapo bunge la nchi hiyo limeidhinisha mswaada wa kupiga marufuku uchinjaji wa paka na mbwa, kwa matumizi ya binadamu.
Katika mswaada huo pia unazuia wote wanaotumia gari au pikipiki kuwavuta wanyama wao wa kuchezea, au kuwatanguliza wanaposafiri.
Yeyote atakayepatikana akikiuka amri hiyo, atakabiliwa na faini kubwa au kufungwa hadi miaka miwili jela - na majina pamoja na picha zao kuwekwa hadharani.
Hayo yote yamefanyika kama jitihada za kuboresha sheria za kuwalinda wanyama nchini humo.
Hatua hiyo ya Jumanne wiki hii, ni mabadiliko makubwa mno ya kuwalinda wanyama nchini Taiwan, na ni moja ya aina yake kuanza kutekelezwa barani Asia.
Mwaka 2001, Taiwan ilipitisha sheria ya kupiga marufuku uuzaji wa nyama na manyoya ya wanyama wa kuchezea kama vile paka na mbwa, kwa kile kilichotajwa "madhumuni ya kiuchumi".
Nyama ya mbwa, zamani ilitumika kwa mara katika kisiwa hicho kama chakula, lakini kwa sasa mnyama huyo anafaa kujumishwa kama mmojawepo wa wanafamilia.

No comments

Powered by Blogger.