-->

Header Ads

2FACE MATATANI KWA WIZI

Huenda hakuna wimbo mwingine mkubwa zaidi Afrika unaompa sifa mwanamke wa Kiafrika kama ule wa Innocent Idibia "2 Face", African Queen. Ni wimbo ambao kwa asilimia kubwa umekuwa ni nembo ya uzuri wa Afrika na wanawake wote kwa ujumla.

Wimbo mwingine mkubwa sana katika historia ya 2 Face/ 2 Baba ni wimbo "Let Somebody Love You" ambao ulishirikisha vocals za msanii Bridget Kelly. Bridget ni msanii ambaye amesaini chini ya leboya Rock Nation inayomilikiwa na msanii nguli wa Hip Hop, Jay Z.

2 Face anatuhumiwa kuuiba wimbo huo kutoka kwa msanii Black Face ambaye alikua mwanabendi mwenzake miaka ya 2000. Black Face anamtuhumu 2 Face na meneja wake kwa kujaribu kumzima kwenye tasnia baada ya kuiba wimbo wake.

 Burudika na wimbo unaoleta mgogoro kati ya Black Face na 2 Face, LET SOMEBODY LOVE YOU.
 
 JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA
 Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.