-->

Header Ads

Vanessa Mdee Atakiwa Tena Polisi Jumatano hii


Baada ya kuachiwa kwa dhamana Jumatatu hii, Vanessa Mdee atakiwa kuripoti kituo cha polisi cha kati (Central) Jumatano hii.


Kwa mujibu wa maelezo ambayo Bongo5 imepatiwa kutoka kituoni hapo, hitmaker huyo wa Cash Madame ameachiwa kwa dhamana Jumatatu hii, baada ya kufanyiwa mahojiano ya mwisho hiyo jana.


Mrembo huyo amekuwa akishikiliwa na jeshi la polisi tangu Jumatano iliyopita. Vanessa ni miongoni mwa mastaa waliotajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana kuhusishwa na matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

No comments

Powered by Blogger.