TETESI : MAN UTD YAJIPANGA KUMSAJILI OZIL, CHELSEA YAWEKA DAU KWA AJILI YA COMAN
Mesut Ozil Arsenal 2017
Manchester United wanajiandaa kumsajili mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil kwa mujibu wa Football.London.
Mjerumani huyo anamaliza mkataba wake na washika mtutu wa London mwisho wa msimu ujao na hajafikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya.
Hali hiyo imemfanya Jose Mourinho aone kama ataweza kumpata mchezaji huyo kirahisi kwani alishafanya naye kazi akiwa Real Madrid.
VERRATTI ANATAKA KUONDOKA PSG
Verratti Barcelona PSG
Marco Verratti amemuelekeza wakala wake kumtafutia klabu nyingine kwani anataka kuondoka Paris Saint-Germain majira ya joto, kulingana na Mundo Deportivo.
Muitaliano huyo amekerwa na timu hiyo baada ya kutolewa kirahisi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa mikononi mwa Barcelona, na magazeti yanadai kuwa maisha yake binafsi pia yanamsukuma kuondoka Paris.
Barcelona, Juventus na Bayern Munich zote zilishaonyesha nia ya kumtaka Verratti na huenda mojawapo ikamsajili majira ya joto.
CHELSEA YAWEKA DAU KWA AJILI YA COMAN
Kingsley Coman Bayern Munich
Chelsea imetoa dau la €60 millioni kwa ajili ya winga wa Juventus Kingsley Coman, kwa mujibu wa Telefoot via Get French Football News.
Coman kwa sasa anatumikia mkataba wa miaka miwili wa mkopo Bayern Munich, kwa makubaliano ambayo yatamruhusu kuhamia kwa mabingwa hao wa Bundesliga kwa uhamisho wa kudumu kwa kitita cha €20m.
Lakini Blues wanaamini watafanikiwa kumshawishi Mfaransa huyo kutua kwenye Ligi ya Uingereza ingawa Manchester City nao wameshatoa dau la €50m kwa ajili ya winga huyo
No comments