-->

Header Ads

HAKUNA UBISHI: Kikosi cha Mayanga Kilipaswa kuwa na NYOTA HAWA pia

rafael-daudi-mbeya-city

Kuna baadhi ya wachezaji hawajajumuishwa kwenye kikosi cha Mayanga licha ya kuwa na msimu mzuri kwenye Ligi Kuu Bara

Kocha wa timu ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga amewaita wachezaji 26 kwa ajili ya mechi za kirafiki na zile za kuwania tiketi ya Chan na AFCON 2019.

Hakuna mabadiliko makubwa kwenye kikosi hicho, asilimia kubwa sura zikiwa ni zile zile, ni Mbaraka Yusufu na Abduraham Musa ndiyo maangizo mapya, halikadhalika Hassan Kessy, Salum abboubakar, Domayo, Ndemla, Said Mohamed, Salim Mbonde, wakirejeshwa baada ya kipindi kirefu kuwa nje ya timu ya taifa.

“Nimechagua wachezaji kulingana na uwezo" - Salum Mayanga

Kwa ujumla kikosi alichoteua Mayanga kinaundwa na Makipa; Aishi Manula (Azam), Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Mabeki; Shomary Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Yanga), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba), Gardiel Michael (Azam), Andrew Vincent (Yanga), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam FC).

Viungo ni Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam), Said Ndemla (Simba), Frank Domayo (Azam), Muzamil Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (DC Tennerife) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden), Ibrahim Hajib (Simba), Mbarak Yussuf (Kagera Sugar) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).

Kuna baadhi ya wachezaji hawajajumuishwa kwenye kikosi cha Mayanga licha ya kuwa na msimu mzuri kwenye Ligi Kuu Bara.

Goal inakuletea wachezaji ambao walistahili kuwepo kwenye kikosi cha timu ya Tanzania, taifa stars chini ya Mwalimu Mayanga.

Mohamed Ibrahim" Mo"

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Mo amekuwa mmoja wa viungo bora ndani ya Ligi Kuu, uwezo wa mkubwa wa kutengeneza nafasi kwa wenzake na kufunga, ni kiungo wa aina tofauti ya viungo wengi hapa nchini.

Salumu Kimenya

Alistahili kuwepo mbele ya Erasto Nyoni wa Azam na Andrew Vincent wa Yanga, mlinzi huyu wa kati wa Tanzania Prisons ya Mbeya, amekuwa na msimu mzuri mpaka sasa ameifanya klabu yake kuwa ni mmoja ya timu zenye nguzo imara.

Kenny Ally
Licha ya kucheza kiungo mkabaji Kenny Ally amehusika kwenye magoli zaidi ya saba Ligi Kuu, kwa kufunga au kuchangia kwa wenzake, chini ya Kinna Phiri kiungo huyu amekuwa bora zaidi, ni mzuri kwenye ulinzi na kupandisha timu pindi timu ikiwa inafanya hivyo.

Raphael Daud
Ndiye kiungo mwenye magoli mengi ya kufunga Ligi Kuu, amehusika kwenye magoli zaidi ya 13 ndani ya klabu yake ya Mbeya City, amefunga magoli 8 magoli manne nyuma ya kinara wa mabao Msuva

No comments

Powered by Blogger.