-->

Header Ads

MFAHAMU GAIDI WA LONDON ALIYEUWA KIPEKEE

Mtu aliyefanya hujuma ya kigaidi hivi karibuni mjini London karibu na bunge na kuua watu wanne aliwahi kuwa mwalimu wa Kiingereza nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la Uingereza, Khalid Masood alifungwa jela mara ya kwanza mwaka 1983 akiwa na umri wa miaka 19 na aliwahi kupatikana na hatia ya vitendo kadhaa vya jinai hadi mwaka 2003. Baada ya hapo alipata cheti cha TESOL cha kufunza lugha ya Kiingereza kwa wazugumzaji wa lugha nyinginezo.

Cheti hicho kilimuwezesha kupata kazi ya kufunza Kiingereza nchini Saudi Arabia katika mji wa Yanbu mwaka 2005. Baada ya hapo alijiunga na Shirika la Usafiri wa Anga Saudi Arabia (GACA) mjini Jeddah.  Alirejea Uingereza mwaka 2009 na kuendelea na kazi ya kufunza lugha ya Kiingereza.



Shirika la Usalama wa Ndani Uingereza MI5 linasema Masood aliwahi kuchunguzwa kutokana na misimamo mikali ya kufurutu ada na tabia za utumiaji mabavu. Masood aliyekua na umri wa miaka 52 alijulikana kwa majina ya Adrian Elms na Adrian Ajao kabla ya kusilimu. Mbali na watu wanne waliouawa katika hujuma hiyo ya London, Masood mwenyewe naye aliuliwa na vikosi vya usalama katika tukio hilo baada ya kuua watu hao wanne. Kundi la kigaidi la ISIS limedai kuwa shambulio hilo limefanywa na mfuasi wake.

No comments

Powered by Blogger.