MICHEZO : JUVE WANAITAKA BARCA SIO BAYERN
Juve wanaamini Bayern Munich ni timu hatari zaidi, hivyo Bonucci anatamani kukutana na Barcelona katika droo itakayopigwa Ijumaa
Beki wa kati wa Juventus Leonardo Bonucci amesema kuwa angependa kukutana na Barcelona kwenye mechi za robo fainali Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Juventus imefanikiwa kutinga robo fainali baada ya kuitoa Porto kwenye michuano hiyo, na Bonucci anatamani droo ya Ijumaa iwakutanishe na Barca ili walipize kisasi cha 2014-15 dhidi ya timu hiyo inayonolewa na Luis Enrique.
"Klabu yetu ni miongoni mwa klabu bora za Ulaya na sasa ni muda wa kwenda mbali iwezekanavyo. Leicester imeshangaza wengi katika michuano lakini mimi binafsi ningependa kukutana ba Barcelona," alisema Bonucc, kwa mujibu wa tovuti ya klabu hiy.
"Kukutana na klabu iliyotunyima fursa ya taji miaka miwili iliyopita litakuwa jambo la maana kubwa kwetu. Baada ya kuishangaza PSG, naweza kusema katika timu zilizobaki Barca wapo katika hali nzuri na wanajiamini.
"Ambaye hatutaki kukutana naye? Bayern Munich. Kila tunapokwenda [Carlo] Ancelotti anajua namna ya kushinda, kama Guardiola. Ni vema kukutana na Bayern kwenye mechi moja tu ya fainali ambapo jambo lolote linaweza kutokea."
Juve kwa sasa wanaongoza ligi ya nyumbani katika msimamo wa Serie A, wakiwa na jumla ya pointi 70 katika mechi 28.

No comments