KUNA "SHAKA" KATIKA MAAMUZI HAYA
Na Charles Francis M,
Siku ya Jumamosi tarehe 11.07.2015, walio kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Sophia Simba, Emmanuel Nchimbi na Adam Kimbisa walitoka nje ya ukumbi wakipinga utaratibu wa kuengua majina ya wagombea Urais kwa tiketi ya chama hicho.
Walipo fika nje, kundi la waandishi wa habari lililo piga kambi Dodoma wakati huo, liliwalaki likitaka kujua nini kina endelea na jambo gani limewatoa nje ya ukumbi kabla ya muda rasmi.
EMMANUEL NCHIMBI alikuwa mzungumzaji mkuu katika "press" ile. Akina Adam Kimbisa na Sophia Simba walikuwa waki-support maelezo ya Nchimbi kwa vyombo vya habari. Nchimbi alieleza umma wa Watanzania kupitia wana habari kuwa haki na misingi ya demokrasia imekiukwa kwa kiasi kikubwa hivyo wao (watatu) hawakubali.
HOJA ZIKO HAPA:
1. Emmanuel Nchimbi alionekana kuwa mzungumzaji mkuu siku ile mbele ya waandishi wa habari. Lakini katika hukumu ya leo, chama cha mapinduzi kimempa onyo kali. Ikumbukwe kuwa huyu Nchimbi baadae aliteuliwa kuwa balozi nchini Brazil na Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi.
2. Usaliti wa Sophia Simba ulio igharimu CCM na kupelekea hukumu kali ya leo, ni upi?? Kwa sababu kama ni usaliti hata Nchimbi ni msaliti lakini kwanini hukumu nzito iwe juu ya Sophia Simba??
3. Kwanini adhabu ziwe tofauti katika kosa moja ikiwa msingi wa kosa ni usaliti?? Yaani wote watatu ni wasaliti lakini hukumu tofauti!! Kwamba Sophia Simba ni msaliti zaidi??
4. Je, tuamini kuwa walio kuwa wafuasi wa Lowassa sasa wana shughulikiwa?? Ikiwa ndiyo, kwanini kuna viashiria vya wengine kuachwa??
5. Mama Salma Kikwete kugombea nafasi (UWT) itakayo achwa wazi na Sophia Simba??
6. Je, Mama Sophia Simba amepigwa rungu kubwa kwa sababu hana ushawishi tena ndani ya chama cha mapinduzi?? Kwamba Kimbisa na Nchimbi wana ushawishi na mtandao mpana ndani ya chama??
7. Kimbisa ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Dodoma. Huu ni mkoa ambao kwa muda mrefu umekuwa ngome ya CCM na majimbo yote yako chini ya CCM. Ni mkoa ambao Spika wa bunge, Job Ndugai anatokea. Kuna kila dalili kuwa Kimbisa ana mtandao mpana sana katika chama hususani katika mkoa huo. Je, ushawishi wake na nguvu hiyo yamkini imeogopwa kukinusuru chama na mpasuko??
NB: Sophia Simba amepoteza sifa ya kuendelea kuwa mbunge wa viti maalum vile vile nafasi yake ya uenyekiti wa UWT (taifa) mpaka sasa iko wazi.
"Caytano Maytano"
Charles Francis M.
No comments