-->

Header Ads

ALI KIBA NA DIAMOND KUSHIRIKI PAMOJA NYIMBO YA KUHAMASISHA SERENGETI BOYS

KUELEKEA fainali ya kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 nchini Gabon, kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys inayoongozwa na Mwenyekiti Charles Hilal imeandaa wimbo wa pamoja utakaoimbwa na wasanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Naseebb Abdul ‘Diamond’ na Ali  Saleh ‘King Kiba' pamoja na wasanii wengine.

Wimbo huo wa pamoja ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha kampeni za kuchangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys itakayofanyika mwezi wa tano nchini Gabon ambapo zitapatikana nchi nne zitakazokwenda kombe dunia la vijana nchini India.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Charles Hilal amesema kuwa kwa pamoja wimbo utakaowahusisha wasanii wengine mbalimbali utakuwa na lengo kuu la kuhamasisha wananchi, wadau na wapenda michezo kuichangia timu hiyo ya vijana kwa lengo la kuisaidia malengo waliyokuwa wameyafikia ya kuipeleka timu hiyo kwenye fainali za kombe la Dunia nchini India.

Hilal amesema kuwa hatua hii ya kusaidia Serengeti Boys kutawajenga vijana hawa kufanya vizuri katika michuano ya mataifa Afrika kwa vijana ikiw ani pamoja na kupata kambi nje ya nchi na kuchgeza mechi kadhaa za kirafiki kutoka nchini jirani lakini hata hivyo bado wanafikria kutafuta mechi ya kirafiki itakayochezwa hapa hapa Jijini Dar es salaam ikiwa ni kwa ajili ya kuwaaga kuelekea nchini Gabon.

Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge amesema kwamba tayari ala za wimbo huo zimekwishatengenezwa na wasanii hao wote wametumiwa kwa ajili ya kuingiza sauti, ili mara moja wimbo huo ukamilishwe na kuanza rasmi kusaidia kampeni ya kuhamasisha Serengeti Boys.

“Tayari wasanii Ali kiba na Diamond wameshakubali kurekodi nyimo hiyona wameahidi kufanya haraka kuingiza sauti kwenye ala ambazo tumeshawatumia na baadae wasanii wengine kama Mwasiti Almasi, Darasa na Vanesa Mdee nao wataweka sauti zao,"amesema Kitenge.

Kiba na Diamond wote wapo kwenye Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ya kuhamasisha na kuwaunganisha Watanzania kwa pamoja ili kuichangia Serengeti Boys iliyofuzu Fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu.

Katibu wa Kamati hiyo ni Mwesigwa Selestine ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati wajumbe ni Kitenge wa EFM Radio na TV, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano na Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu, yumo Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas, Mkurugenzi wa Global Publishers Limited, Eric Shigongo na Mkurugenzi wa Radio Clouds, Ruge Mutahaba.

Pia, Serikali iliridhia kuwa mshiriki wa karibu kwa kila hatua kuanzia Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya timu za taifa, Kamati ya Hamasa kwa lengo la kupanga pamoja na kushirikiana kwa pamoja.
Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya Serengeti Boys kueleka kwnye kombe la Mataifa Afrika chini ya miaka 17 yatakayofanyika nchini Gabon. Kushoto ni Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano 
Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal akiwa pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge wakiwasikilizisha waandishi ala za wimbo unaotarajiwa kutumika kwa ajili ya kuhamasisha kuichangia Serengeti Boys.

No comments

Powered by Blogger.