Afrika Kusini yaunga mkono mpango wa kuasisiwa nchi huru ya Palestina
Afrika Kusini imesisitiza kuwa inaunga mkono suala la kuasisiwa nchi huru ya Palestina ili kuhitimisha mzozo wa Mashariki ya Kati.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema kuwa suluhisho la kuunda nchi mbili zilizo huru ni njia pekee inayoweza kuupatia ufumbuzi wa kudumu mzozo wa Mashariki ya Kati.
Akihutubia Bunge la Afrika Kusini kwa mara ya kwanza mwaka huu, Rais Zuma ameeleza kuwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na Israel katika ardhi za Palestina utakwamisha juhudi za jamii ya kimataifa za kutekeleza makubaliano ya Oslo na kupata ufumbuzi wa kuuasisi nchi mbili huru.
Rais wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa, kuna udharura wa kufanikisha mchakato wa kuundwa nchi mbili huru na hivyo kuhitimisha mzozo katika eneo la Mashariki ya Kati.
Utawala wa Kizayuni unajenga nyumba mpya zaidi ya elfu nne katika ardhi unazozikalia kwa mabavu za Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na huko Baitul Muqaddas Mashariki ukisaidiwa na Rais wa Marekani.
Rais Jacob Zuma ameongeza kuwa, raia wa Palestina wanaishi katika mazingira ya kusikitisha ykwa miaka 50 sasa tangu nchi yao ikaliwe kwa mabavu na Israel. Amesema Afrika Kusini inasisitiza uungaji mkono wake kwa juhudi za kimataifa zinazotaka kuasisiwa nchi huru ya Palestina.

Nyumba mpya za walowezi wa Kiyahudi zinazoendelea kujengwa na Israel katika ardhi za Wapalestina
|

No comments