ABDUL NONDO AICHAMBUA SIRI ILIYOPO UTATA WA KAMPUNI YA MINJINGU MINES NA COUNTY BUNGOMA
Mbunge wa serikali ya wanafunzi CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM 'Abdul NONDO' ametoa maoni yake kuhusu MINJINGU MINES AND FERTILIZER LTD VS BUNGOMA COUNTY GOVERNMENT FERTILIZERS kama ifuatavyo..
'Sasa hivi kila mtu anajiuliza kwanini Mbolea ya minijingu inayozalishwa na minjingu mines and fertilizers LTD, iliyopo TANZANIA na huzalisha mbolea hiyo kwa kutumia malighafi kutoka kwetu TANZANIA ambayo ni madini ya phosphates yaliyopo manyara (mgodi)
Lakini Jambo la kushangaza hapa ni vifungashio hivyo kuandikwa BUNGOMA COUNTY GOVERNMENT FERTILIZERS Nairobi kenya.
Hadi sasa Hakuna anaye fahamu kwanini wamefanya hivyo, lakini director wa minijingu Hans Tosky anasema kuwa wa wateja wao ndio wanapenda kuona vifungoshio vya namna hiyo. ambayo ni sababu ambayo haipo wazi kwanini.
BUNGOMA COUNTY ni mji uliopo Kenya mpakani wa Uganda upande wa magharibi wa Kenya (kaunti ya bungoma) huu mji una serekali ambayo ni jimbo kiongozi huwa ni governor hii ni kwa sababu Kenya bunge lao ni BICAMERAL, mji wa bungoma unajishuhulisha saana na kilimo, biashara, na hata viwanda vya miwa. hadi sasa haijulikani kwa nini MBOLEA YA TANZANIA IANDIKWE Bungoma government county fertilizers ingawa uchunguzi unafanyika lakini yafuatayo yanawezekana ya kawa ni sababu ya haya.
Kenya kumukuwa na kampeni kubwa ya kutoa ya punguzo nafuu kwa wakulima wake ambao hawana uwezo, na wajane wamekuwa wakipewa bure mbolea hiyo (subsidized fertilizers) ,na serekali ya BUNGOMA imekuwa mstari wa mbele wa kutekeleza haya, governor KEN LUSAKA amekuwa mstari wa mbele.
Kwa tatizo hili kuna uwezokano mkubwa kumefanyika CONTRACTING MANUFACTURING,(uzalishaji wa mkataba),huu ni aina ya mkataba ambao unaingiwa Kati ya Kampuni na mzalishaji (hiring firm and manufacturer) kuzalisha bidhaa kwaniaba ya kampuni hiyo kwa kwa makubaliano ya bei ambapo msambazaji na mtafuta soko ni kampuni hiyo.
hapa kuna uwezekano mkubwa Kenya kuna kampuni au hata serekali ya Bungoma kuwa imeingia makubaliano na mkataba na Minijingu mine and fertilizer Ltd kuwa kama mzalishaji yaani manufacturer wa kwa makubaliano yao ya bei, na hiyo kampuni ya bungoma county au hata serekali ya bungoma kuwa msambazaji mkubwa wa mbolea hiyo, kwa kupokea tenders mbali mbali.kwa sababu tuu serekali ya Kenya imekuwa ktk kampeni kubwa ya kugawa mbolea kwa wakulima na ndio maana wananchi wa manyara wamekuwa wakilalamika na hata Waziri Mkuu alisema kuwa wananchi hao hawauziwi hiyo mbolea badala yake wanaagiza nje, hii ni kwasababu anazalisha kwa ajili ya kampuni fulani,kwa ajili ya watu fulani.
Katika mkataba huwa makubaliano yanaweza kuwa minijingu mine and fertilizer limited chini ya TOSKY HANS aandike jina jina hilo.
mambo mengi yanaweza husika humo mfano ukwepaji wa kodi(export tax) , soko, ndio maana kuna uchunguzi lakini haya yanawezekana kabisa Na Kama wakibainika na shutuma yeyote wachukuliwe hatua kali ili kukomesha tabia hiyo sababu hatutaweza kujitangaza kimataifa na tukasifika,pia hatutaweza kuwa na soko.
Pia tunakosa kodi (export tax), ambayo Kenya ndio wanayoipata sababu order zote huishia Kenya.
Shukrani'
Abdul Omar Nondo .
0659366125
Nikweli kuwa kawanda kilikusudia kukwepa kodi lakin nadhan kwakuwa wananchi wa count ya bungoma wanapewa msaada wa mbolea basi selikali ya tanzania ingekosa tax collections .anadhan mmiliki wa kiwanda angebanwa zaikaiandaa kuogopwa Walla kufinya jicho assume kusudi lilikuwa no mini.
ReplyDelete