-->

Header Ads

Zitto Kabwe AINGILIA KATI GODBLESS LEMA Kunyimwa Dhamana


Baada ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania iliyokaa Arusha kutupa Rufaa zote mbili zilizofunguliwa
 na Serikali dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuhusiana na dhamana 
ya mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo,
 Zitto Kabwe amezungumza.

Kiongozi huyo wa ACT ametumia Facebook kutoa malalamiko yake:
Mnamkamata mtu kwa kosa lenye dhamana. Mahakama Kuu inaruhusu dhamana. 
Serikali inakataa rufaa kuzuia dhamana. Mtu anakaa jela miezi 4, tena mwakilishi wa watu. 
Siku ya hukumu kuhusu dhamana Serikali inaondoa shauri mbele ya jopo la majaji 3. Lengo? 
Kumkomoa mtu. Siasa za ukomoaji zinajenga chuki kwenye jamii na chuki inazaa visasi. 
Haitoshi majaji kukemea Ofisi ya DPP. Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha 
mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. 
Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi
 ya wananchi

HASHIM RUNGWE NAE AFUNGUKA.....

Lema Yupo Gerezani Kwa Sababu Isiyo na Msingi..Ila 

Hawajui Wanazidi Kumkomaza Kisiasa-Rungwe

Mwenyekiti  wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashim Rungwe, amemtembelea 
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), ambaye   bado yuko mahabusu katika
 Gereza la Kisongo mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari  mjini Arusha jana baada ya kuonana na mbunge huyo,
 Rungwe alisema baadhi ya matatizo yanayotokea kwenye jamii yanasababishwa na baadhi ya 
watawala.

Alisema hali hiyo imekuwa ikiibua chuki miongoni mwa wananchi   jambo ambalo si zuri na
 linahitaji kukemewa.

Kiongozi huyo alimtembelea Lema    akiwa  amefuatana  na viongozi mbalimbali akiwamo 
Makamu Mwenyekiti wa Chauma, Kayumbo Kabutali  na wabunge wa Bukoba Mjini, 
Wilfred Lwakatare na Moshi Vijijini, Antony Komu,  wote wa Chadema

No comments

Powered by Blogger.